COPA AMERICA : COLOMBIA YATANGULIA ROBO FAINALI,MAREKANI YAITUMBUA COSTA RICA.

Colombia imekua timu ya kwanza kutinga hatua ya Robo fainali ya michuano ya Copa America inayoendelea nchini Marekani.


Kiungo wa Real Madrid James Rodriguez alifunga bao moja na kutengeneza lingine la pili ambalo lilifungwa na Carlos Bacca wakati Colombia wakiifunga Paraguay bao 2-1

Katika mechi nyingine Marekani ambao ni wenyeji waliifunga Costa Rica kwa bao  4-0 magoli ya Clint Dempsey,Jermaine Jones, Bobby Wood na Graham Zusi aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Bobby Wood.

Kwa matokeo haya Colombia wanatinga hatua ya Robo fainali wakiwa na pointi 6 tayari huku Marekani wao wakiwa na pointi 3 na kuhitaji sare tu katika mechi ya mwisho dhidi ya Paraguay.

No comments

Powered by Blogger.