MAJONZI : ALIYEKUA KOCHA WA NIGERIA STEPHEN KESHI AFARIKI DUNIA

Mchezaji wa zamani wa Nigeria ambaye amewahi pia kuifundisha timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles Stephen Keshi amefariki dunia.



Taarifa za msiba huo uliotokea leo Jumatano tayari zimethibitishwa na chama cha soka cha Nigeria NFF.

Keshi amefariki ghafla kwa tatizo la moyo  nyumbani kwake Nigeria.

Keshi aliichezea Nigeria michezo 64 tangu mwaka 1981 mpaka 1995 na alikua mmoja kati ya wachezaji waliotwaa kombe la mataifa ya Afrika mwaka 1994 mwaka ambao Nigeria ilifika nafasi ya 5 Duniani katika viwango vya ubora vinavyotolewa na FIFA ikiwa ndilo taifa la Kwanza Afrika kufikia nafasi hiyo.


Baada ya kustaafu soka Keshi alihamia katika ukocha na kuweza kuzifundisha timu za taifa za Mali,Togo na Kuiongoza tena Nigeria kutwaa kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 safari hii akiwa kama kocha mkuu.
Kabla ya kifo chake Keshi alikua akitajwa kuchukua nafasi ya ukocha wa timu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini. 
Mke wake alishafariki mwaka jana na ameacha watoto wanne. 
UPUMZIKE KWA AMANI JEMBE 

No comments

Powered by Blogger.