CHIRWA SASA RUKSA KUITUMIKIA YANGA
Hatimae uongozi wa Yanga umekamilisha taratibu zote muhimu zitakazo muwezesha mchezaji wao mpya wa kimataifa wa Zambia Obrey Chirwa kuanza kuitumikia klabu hiyo ambayo ni mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara.
Mkuu wa kitengo cha habari cha Yanga Jerry Muro amesema Chirwa anatarajiwa kuondoka Dar es Salaam leo saa sita za usiku kwenda uturuki ambako timu hiyo imeweka kambi ya muda.
Kuwasili kwa Chirwa katika kambi ya Yanga Kutaongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ambayo juzi ilipoteza mchezo wake wa kwanza katika hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika wakifungwa kwa bao 1-0 dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.
Chirwa alisajiliwa na Yanga akitokea Platinum Stars ya Zimbabwe ambaye anatarajiwa kuleta tofauti kama alivyofanya Donald Ngoma.
Mechi ijayo Yanga itacheza dhidi ya Vinara wa kundi ambao ni mabingwa wa Afrika TP Mazembe ya Congo DR

No comments