BAADA YA ENGLAND KUAMBULIA SARE JANA SHUGHULI LEO IKO KWA UJERUMANI

Michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya iliyojulikana kama Euro 2016 inaendelea nchini Ufaransa na leo kutapigwa mechi 3 kuanza Sa10 jioni kwa muda wa Afrika Mashariki



Tuliweza kushuhudia mechi tatu jana ambapo Katika Kundi A Albania walikubali kufungwa bao 1-0 na Uswiss katika mechi ya awali badae Gareth Bale akaiongoza Wales kuifunga Slovakia bao 2-1 na mechi ya mwisho usiku England Ikatoka  sare ya bao 1-1 na Russia katika Kundi B.

Uturuki itacheza na Croatia katika mchezo wa awali leo kuanzia Saa 10 kamili jioni kwa Saa za Africa Mashariki mchezo wa kwanza katika Kundi D ambalo linajumuisha timu za Croatia,Uturuki, Czech Republic na Spain ambao ndiyo mabingwa watetezi

Mechi nyingine leo mabingwa wa dunia Ujerumani watakua uwanjani kucheza dhidi ya Ukraine katika mechi itakayoanza Saa 4 kamili usiku huku Poland Ikicheza dhidi ya Ireland kaskazini mechi itakayoanza Saa 1 kamili usiku.

No comments

Powered by Blogger.