NI MANJI NA SANGA KWA MARA NYINGINE TENA YANGA
Mabingwa wa Tanzania bara na wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa Yanga jana walikamilisha zoezi la uchaguzi wa viongozi wake ambapo Mwenyekiti Yusuph Manji na makamu wake Clement Sanga walirejea madarakani.
Uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanachama lukiki ulimchagua tena bwana Yusuph Manji kuwa mwenyekiti kwa kipindi kingine cha miaka minne kwa kupata kura 1,468 kati ya 1,470 zilizopigwa huku kura mbili tu zikiharibika na hakukuwa na kura ya hapana ikumbukwe kwamba bwana Manji hakuwa na mpizani kwenye nafasi hiyo.
Makamu mwenyekiti Clement Sanga ambaye alikuwa akipigania nafasi hiyo na Titus Osoro ameweza kutetea nafasi yake baada ya kuibuka mshindi kwa kujizolea kura 1,428 kati ya 1,508 zilizopigwa huku Mpinzani wake akiambulia kura 80 tu.
Nafasi za ujumbe wa kamati kulikua na Wagombea 20 na hawa ndiyo walioibuka na ushindi katika uchaguzi:
1. Siza Augustino Lymo (kura 1027)
2. Omary Said Amir (kura 1069)
3. Tobias Lingalangala (kura 889)
4. Salim Mkemi (kura 894)
5. Ayoub Nyenzi (kura 889)
6. Samuel Lucumay (kura 818)
7. Hashim Abdallah (kura 727)
8. Hussein Nyika (kura 770)
Idadi ya wajumbe 12 wameshindwa kuibuka na ushindi baada ya Kura walizopata kushindwa kuwazidi wale walioshinda. Ambao ni
1. David Luhago (582)
2. Godfrey Mheluka (430)
3. Ramadhani Kampira (182)
4. Edgar Chibura (72)
5. Mchafu Chakoma (69)
6. George Manyama (249)
7. Bakari Malima (577)
8. Lameck Nyambaya (655)
9. Beda Tindwa (452)
10. Athumani Kihamia (558)
11. Pascal Lizer (178)
12. Silvester Haule (197)
No comments