YANGA USO KWA USO NA STAND UNITED SHINYANGA LEO
Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga ya Dar es Salaam leo itakua dimbani katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga kuoneshana kazi na Chama la Wana Stand United ya huko.
Yanga ambayo inaendelea na kampeni yake ya kutaka kuutetea ubingwa wake na ikitaka pia kuendelea kuweka wigo wa pointi na wanaoshika nafasi ya pili Azam FC.
Yanga itaingia katika mchezo wa leo jioni ikiwa na kumbukumbu nzuri kabisa ya ushindi mfululizo katika ligi kuu ikishinda pia mechi yake iliyopita dhidi ya Toto Africans kwa bao 2-1 katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.
Wenyeji Stand United mambo yao bado hayajatulia kwani wameendeleza wimbi La kugawa pointi huku walilambishwa bao 1-0 katika mchezo uliopita dhidi ya Mwadui katika mechi iliyochezwa katika dimba La Mwadui Complex.
Katika mechi ya awali baina ya timu hizo Yanga iliwafunga wapiga debe hao wa Shinyanga kwa bao 4-0 hiyo ilikua Disemba 19 magoli ya Yanga yakifungwa na Thaban Kamusoko na Amiss Tambwe aliyefunga hat trick.
Yanga inaongoza hivi sasa katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 65 huku Stand United wao wakiwa na pointi 34 katika nafasi ya 7.

No comments