DAVID DE GEA AWEKA REKODI MPYA MAN UNITED

Kipa namba moja wa Manchester United Mspaniola David de Gea ameweka rekodi mpya katika klabu yake jana usiku baada ya kuwa Mchezaji wa kwanza Klabuni hapo kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa mara ya 3 mfululizo.


Kwenye ya kutoa tuzo mbalimbali kwa msimu huu klabubhiyo iliandaa hafla maalumu na Dabid De Gea ambaye mchango wake ndani ya Man United msimu huu ndiyo kichocheo cha kupata Tuzo hiyo ambayo imepewa jina la lejendari wa timu hiyo Sir Bobby Chalton.

Ukiacha David De Gea Chris Smalling aliyekua pia Tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa kuwa za wachezaji wenzake.

Antony Martial ambaye ni msimu wake wa kwanza kuichezea Manchester United yeye alietwaa Tuzo ya goli bora la mwaka kwa goli lake la kwanza aliloifungia Man United dhidi ya Liverpool.

Kwa upande wa kikosi cha vijana chini ya miaka 21 Beki wa pembeni Cameron Borthwick-Jackson ameshinda mchezaji bora wa mwaka chini ya miaka 21.

Marcus Rashford ambaye amepata nafasi ya kuaminiwa katika kikosi cha Luis Van Gaal ameshinda Tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu hiyo kwa kikosi cha vijana chini ya miaka 18.


No comments

Powered by Blogger.