YANGA HII SASA SIFA : YAZOA VIKOMBE VYOTE TANZANIA BARA KILICHOWAKUTA AZAM LEO NOMA
Wawakilishi pekee wa Tanzania na Afrika mashariki katika michuano ya kimataifa Yanga imeendeleza dozi na kuzoa makombe baada ya leo kutwaa ubingwa wa kwanza wa kombe la Azam Federation Cup.
Yanga imetwaa ubingwa huo wa kwanza baada ya kurudishwa upya kwa michuano hiyo ambayo zamani ilikua ikijulikana kama kombe la FA kwa kuwafunga wanalambalamba Azam FC kwa bao 3-1.
Amiss Tambwe alitangulia kuipatia Yanga bao la kwanza dakika ya 10 ya mchezo kabla ya kuongeza la pili dakika moja baada ya mapumziko kisha Didier Kavumbagu akafanikiwa kuipatia Azam bao pekee dakika moja baada ya Tambwe kufunga bao la pili kisha Deus Kaseke akaifungia Yanga bao la 3 dakika ya 81.
Yanga ikapewa kombe lake ambalo ni la pili msimu huu baada ya lile la ubingwa wa bara na kupata kitita cha milioni 50 toka kwa wadhamini kampuni ya Azam.
Kipa bora wa mashindano hayo ambaye alikabidhiwa zawadi yake ni Aishi Manula wa Azam FC huku mchezaji bora ni Juma Abdul wa Yanga na Atupele Green wa Ndanda akachukua tuzo ya mfungaji bora.
Bingwa wa Mashindano hayo hupata tiketi ya kucheza kombe la shirikisho barani Afrika na kwakua Yanga wameshapata nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa Afrika basi Azam FC ndiyo watachukua nafasi ya Yanga msimu ujao.

No comments