WANYAMA WA SOUTHAMPTON AINYIMA USHINDI STARS DHIDI YA KENYA

Pambano la kimataifa la kirafiki kati ya wenyeji timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars limemalizika kwa sare ya bao 1-1.


Wachezaji wa Stars wakimpongeza Maguli kwa kufunga bao

Pambano hilo lilipigwa katika dimba la Nyayo jijini Nairobi lilishuhudia kiungo wa Southampton ya  England Victor Wanyama akiisawazishia Kenya bao kwa njia ya penati ikiwa ni dakika 6 tu baada ya Elias Maguli kuifungia Taifa Stars kwa kichwa akiunganisha mpira wa beki Juma Abdul.

Stars ilikua ikijiandaa kwaajili ya mchezo dhidi ya Misri wiki ijayo huku Kenya wao wakitarajiwa kucheza na Sudan.

No comments

Powered by Blogger.