SAMATA AWEKA REKODI MPYA BAADA YA GENK KUFUZU EUROPA LEAGUE
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na Nahodha wa kikosi cha Taifa Stars Mbwana Samatta ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza katika michuano ya Europa league.
Samatta akiichezea KRC Genk ya Ubelgiji leo wamepata nafasi ya kucheza michuano hiyo ya pili kwa ukubwa ngazi ya klabu barani Ulaya wakiifunga Charleroi kwa bao 5-1 katika mchezo wa marudiano hatua ya Mtoano ligi kuu ya Ubelgiji katika dimba la Cristal.
Samatta leo alifunga bao moja kati ya mabao hayo matano ya Genk huku Nikos Karelis akifunga mabao matatu peke yake na bao lingine likifungwa na Sandy Walsh.
Kwa matokeo hayo ya leo KRC Genk imeshinda kwa matokeo ya jumla ya mabao 5-3 baada ya kufungwa bao 2-0 mchezo wa awali na katika Europa League msimu ujao wanaweza kukutana na vilabu mashuhuri barani Ulaya kama Manchester United, West Ham na Southampton toka katika ligi kuu nchini England.

No comments