SIMBA MWAKA WA HASARA YAAMBULIA SARE SONGEA

Mambo yamezidi kuwaendea kombe Wekundu wa Msimbazi Simba baada ya kuambulia Sare ya bila kufungana katika mchezo wake dhidi ya Majimaji mjini Songea.



Simba iliingia katika mchezo huo wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa na uhaba wa wachezaji na kupelekea kuwa na wachezaji Watatu tu katika benchi ilijikuta ikibanwa mbovu vilivyo na wanalizombe huku Majimaji wakishindwa wenyewe kufunga baada ya kupata nafasi nyingi

Kocha Jackson Mayanja aliamua kuwatumia wachezaji wa Kitanzania pekee katika mchezo huo kutokana na wachezaji wake wa kigeni kuchelewa kufika Mjini Songea ikisemekana kwamba waliobaki Dar es salaam kufatilia malipo yao.

Simba inaendelea kushika nafasi ya tatu baada ya matokeo hayo ikiwa na pointi 59 point moja nyuma ya Azam wanaokamata nafasi ya pili

No comments

Powered by Blogger.