LIVERPOOL VS CHELSEA HAKUNA MBABE, SUNDERLAND YAZISHUSHA DARAJA NEWCASTLE NA NORWICH
Pambano la ligi kuu nchini England baina ya wenyeji Liverpool dhidi ya Chelsea lilimalizika kwa Sare ya bao 1-1 katika dimba la Anfield jijini Liverpool.
Eden Hazard alitangulia kuifungia Chelsea bao la uongozi dakika ya 32 bao ambalo lilitawala muda wote wa mchezo mpaka Christian Benteke alipoisawazishia Liverpool kwa bao la dakika ya 90 ya mchezo akifunga kwa kichwa.
Katika mchezo mwingine hiyo jana wenyeji Sunderland walijihakikishia nafasi ya kubaki katika ligi kuu ya England msimu huu baada ya kuibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Everton katika uwanja wa Mwangaza.
Mlinzi wa Sunderland Raia wa Ufaransa Lamine Kane ndiye aliyekuwa shujaa wa mchezo huo kwa kufunga bao 2 katika ushindi huo wa bao 3-0 huku bao lingine likifungwa na mlinzi Patrick Van Aanholt
Kwa matokeo hayo Sunderland wamefikisha pointi 38 pointi ambazo zinawahakikishia kubaki katika ligi kuu kwa msimu ujao na sasa kuzifanya Norwich City ambao jana walishinda 4-2 wakiwafunga Watford pamoja na Newcastle United ambao wikiendi walitoka Sare ya bila kufungana na Aston Villa kushuka Daraja wakifunga na Aston Villa ambayo tayari ilishashuka Daraja.
Hata kama Norwich City na Newcastle United watashinda mechi zao za mwisho hawawezi kufikia pointi za Sunderland.
Tumekuwekea Highlights za mechi zote za jana EPL kama hukupata muda wa kuangalia

No comments