LEO KATIKA HISTORIA : SIR ALEX FERGUSON ANAAGWA KWA USHINDI DHIDI YA SWANSEA NA UBINGWA WA 20 KWA MAN UNITED MWAKA 2013

Leo katika historia tunakumbuka siku ambayo Wapenda Soka duniani waliungana na mashabiki wa Manchester United walioujaza uwanja wa Old Trafford kumuaga kocha Alex Ferguson.


Baada ya miaka 26 ya kuitumia Manchester United tarehe kama ya leo mwaka 2013 Kocha Sir. Alex Ferguson kwa hiari yake aliamua kustaafu kufundisha soka akiiwezesha United kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini England kwa mara ya  20 na wa 13 kwake yeye kama kocha wa Manchester United

Siku hiyo ya Jumapili tarehe 12 May 2013 Manchester United Ilicheza mchezo wake wa mwisho wa msimu huo na wa mwisho kwa Sir Alex Ferguson katika dimba la Old Trafford na kukabidhiwa kombe lake dhidi ya Swansea na kuibuka na ushindi wa bao 2-1.

Javier Hernandez Chicharito alifunga bao la kuongoza kwa United kabla ya Michu hajaisawazishia Swansea na baadae beki Rio Ferdinand akafunga bao la ushindi.

VIKOSI


Manchester United

01 De Gea
03 Evra
04 Jones
05 Ferdinand
15 Vidic
16 Carrick
19 Welbeck (Valencia - 66' )
22 Scholes (Anderson - 66' )
26 Kagawa
14 Hernandez (Giggs - 76' )
20 Van Persie

AKIBA

13 Lindegaard
06 Evans
28 Buttner
07 Valencia
08 Anderson
11 Giggs
23 Cleverley

Swansea City

25 Tremmel
03 Taylor (Davies - 65' )
04 Chico
06 Williams
21 Tiendalli
07 Britton
09 Michu (Rangel - 74' )
11 Pablo (Agustien - 87' )
12 Dyer
15 Routledge
20 De Guzman

AKIBA

13 Cornell
16 Monk
22 Rangel
33 Davies
26 Agustien
14 Lamah
17 Shechter
Refa: Moss
Watazamaji: 75,572

No comments

Powered by Blogger.