SIMBA KUIKABILI MWADUI YA JULIO TAIFA.

Baada ya michezo mitatu ya ligi kuu Tanzania bara kupigwa jana leo ni fursa nyingine kwa Wapenda soka kushuhudia michezo mingine mitatu katika viwanja vitatu nchini.



Wekundu wa Msimbazi Simba ambao walijichimbia Zanzibar kujiandaa na mchezo wa leo watakua wenyeji wa Mwadui FC ya Shinyanga timu inayonolewa na Mchezaji na kocha wa zamani wa Simba Jamhuri Kiwelu Julio.

Simba inayokamata nafasi ya pili ikiwa na pointi 58 baada ya Azam kupokea pointi itakua na nia moja tu ya kuibuka na ushindi katika pambano hilo ili kuisogelea Yanga inayokamata nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 68 yani pointi 10 mbele ya Simba

Mwadui wao hawana cha kupoteza japokua ushindi utawapandisha katika msimamo kwakua wanakamata nafasi ya 6 wakiwa na pointi 37 wakihitaji kulinda heshima na kujiweka sawa kwaajili ya msimu ujao.

Mechi ya mzunguko wa kwanza katika dimba la Kambarage mjini Shinyanga timu hizo zilitoshana nguvu kwa kutoka Sare ya bao 1-1 Nizar Khalfan na Brian Majwega wakiwa ni wafungaji siku ya "boxing day".

Katika mechi nyingine hii leo Azam FC wao watakua mjini Shinyanga kuonyeshana nguvu na wenyeji Kagera Sugar ambao wanatumia uwanja wa Kambarage kama uwanja wao wa nyumbani baada ya uwanja wa Kaitaba kuwa katika matengenezo makubwa.

RATIBA KAMILI YA MECHI ZA LEO


  • Kagera Sugar vs Azam FC 
  • Simba SC vs Mwadui FC 
  • Prisons vs Maji Maji FC 







No comments

Powered by Blogger.