AZAM FC USO KWA USO NA KAGERA SUGAR HUKO SHINYANGA LEO
Mabingwa wa soka Afrika Mashariki na Kati klabu ya Azam FC leo itajitupa uwanjani katika moja kati ya mechi 3 za ligi kuu Jumapili ya leo kucheza na wakati miwani wa Kagera klabu ya Kagera Sugar.
Azam FC wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 57 wakati Kagera Sugar wao wako katika nafasi ya 14 wakiwa na pointi 25 tu hii inawaweka katika balaa la kushuka Daraja na ushindi pekee leo utawaweka katika matumaini mapya.
Pambano la awali baina ya timu hizo lililopigwa katika dimba la Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam wenyeji Azam waliifunga Kagera Sugar bao 2-0 magoli ya Kipre Tchetche na Shomari Kapombe.
Tayari kikosi cha Azam kilishasafiri kwa ndege tangu juzi na kuweka kambi jijini Mwanza kujiandaa na pambano hilo jioni ya leo

RATIBA YA MECHI ZOTE ZA LEO
- Kagera Sugar vs Azam FC
- Prisons FC vs Maji Maji FC
- Simba SC vs Mwadui FC
No comments