PEP GUADIOLA AMWAGIWA BIA ZA KUTOSHA WAKATI BAYERN MUNICH WAKIMUAGA

Miaka mitatu ndani ya Allianz Arena kocha Pep Guardiola ameagwa leo kwa ushindi kutetea ubingwa wa Bundesliga huku akishinda pia mechi yake ya mwisho leo dhidi ya Hannover.


Kocha huyo mwenye miaka 45 Raia wa Spain ameiongoza Bayern kutwaa ubingwa wake wa 26 na msimu ujao atatimkia Manchester City huku nafasi yake itachukuliwa na Carlo Ancelotti.

Bayern imeibuka  na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Hannover Shukrani kwa magoli ya Roberto Lewandowski aliyefunga bao 1 likiwa ni bao lake la 30 msimu huu wakati Mario Gotze yeye alifunga bao 2 peke yake.

Baada ya mechi hiyo Bayern walikabidhiwa ngao ya ubingwa na kisha shangwe za kusherekea ubingwa zikafata zikimuhusu sana kocha Pep Guardiola kwani kama ilivyo utamaduni wao walimwagia bia za kutosha katika glass kubwa zinazoingia chura tatu za bia.






No comments

Powered by Blogger.