IBRAHIMOVIC AWAZAWADIA BAO 2 ZA MWISHO MASHABIKI KATIKA DIMBA LA PARC DE PRINCE
Mchezo wa mwisho wa ligi kuu nchini Ufaransa baina ya wenyeji PSG na Nantes uliishuhudia PSG ikiibuka na ushindi mnono wa bao 4-0.
Mchezo huo ulikua pia ni wa mwisho wa ligi kuu nchini Ufaransa kwa Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic katika dimba la Parc de Prince huku akitarajiwa kucheza Mchezo WA mwisho Katika fainali YA kombe La Ligi nchini Ufaransa ambaye ameshatangaza kwamba ataihama klabu hiyo baada ya kumalizika msimu huu.
Mashabiki wa PSG waliujaza uwanja huo kumuaga shujaa huyo ambaye atakumbukwa kwa mchango wake wa kupachika mabao na dakika ya 10 uwanja mzima ulisimama Kumpiga makofi wakitambua mchango wake na jezi yake namba 10.
Shukrani alizotoa kwa mashabiki wake ni kuendelea kufunga na alifunga bao mbili hiyo jana la kwanza akifunga kwa kifua alipounganisha pasi ya Angel Di Maria na la pili kwake akifunga kwa kichwa huku akishiriki katika kutengeneza mabao mengine mawili yaliyofungwa na Lucas Moura na Beki Marquinhos baada ya mpira wa adhabu ndogo wa Ibrahimovic kupanguliwa na kipa wa Nantes.
Wakati mpira ukiendelea watoto wa Ibrahimovic waliingia uwanjani wakiwa wamevalia jezi zenye namba 10 mgongoni moja ikiandikwa King na nyingine Legend wakitimiza maneno aliyeandika Ibrahimovic katika mtandao wa twitter "I came like a king left like a legend"
Magoli aliyofunga jana yanamfanya kufikisha magoli 38 katika ligi msimu huu katika ligi akivunja rekodi ya miaka mingi ya mshambuliaji Carlos Bianch ambaye alifunga magoli 37 msimu wa mwaka 1977-1978.
Ibrahimovic anahisishwa kujiunga na Manchester United msimu ujao.

No comments