MAN UNITED YAMZUIA RASHFORD KWA MKATABA MPYA MPAKA 2021

Kiwango cha mshambuliaji kinda wa Manchester United Marcus Rashford kimepelekea timu hiyo kumpa mkataba mpya wa  miaka minne ambao utamweka klabuni hapo mpaka 2021.


United  imeamua kuwazuia vijana wake toka katika timu yao ya vijana na wameanza kwa kuwapa mikataba wachezaji hao ili washindwe kuihama timu hiyo.

Rashford mwenye miaka 18 amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa awali na katika mkataba huu mpya Rashford atakua akipokea paundi 25,000 kwa wiki kutoka katika mkataba wa awali ambao alikua akipokea paundi 1,300.

Rashford anasimamiwa na kaka yake Dwaine Maynard katika maswala yote ya mkataba mpya na United inatarajia kutangaza rasmi baada ya fainali za Euro 2016

Amekua na msimu mpya na Mashetani wekundu baada ya kufunga bao 8 katika mechi 18 tangu alipoingia katika mechi yake ya kwanza mwezi February dhidi ya Midjitland katika michuano ya Europa league.

Juzi Ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo kabisa kufunga katika mechi yake ya kwanza akiwa na timu ya taifa katika ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Australia.
 

No comments

Powered by Blogger.