DIAME AIRUDISHA HULL CITY LIGI KUU NCHINI ENGLAND

Kiungo wa  kimataifa wa Senegal na klabu ya Hull City Mohamed Diame jana aliibuka shujaa baada ya kufunga bao pekee dhidi ya  Sheffield Wednesday katika mechi ya fainali kutafuta timu ya tatu kupanda daraja la ligi kuu ya England.



Diame alipiga shuti la mbali na kuzama moja kwa moja golini dakika ya 72 ya mchezo huo wa fainali kuwania timu ya mwisho kupanda daraja katika dimba la Wembley jijini London.

Hull City imetumia siku 370 kurejea tena katika ligi kuu baada ya kushuka daraja msimu uliopita.

Hull city itaungana na Burnley na Middlesbrough kupanda daraja msimu ujao zikichukua nafasi za Aston Villa, Newcastle United na Norwich City zilizoshuka daraja msimu huu.

Hii ni mara ya nne kwa kocha Steve Bruce kupandisha timu daraja baada ya kufanya hivyo mwaka 2002 na 2007 akiwa na Birmingham city  na mwaka 2013 na 2016 akiwa na Hull city.

No comments

Powered by Blogger.