LIVERPOOL YAANZA USAJILI : KIPA WA UJERUMANI ASAINI MIAKA MITANO
Kuelekea katika maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu nchini England tayari klabu zimeanza usajili wao na baada ya Arsenal kumsajili Xhaka wiki iliyopita jana ilikua ni zamu ya Liverpool kukamilisha uhamisho wa kipa Loris Karius toka Mainz ya Ujerumani.
Kiasi cha Pauni Milioni 4.7 kimetumika kumsaini Kipa huyo mwenye Miaka 22 anayeidakia pia Timu ya Taifa ya Ujerumani chini ya Miaka 21 na amekabidhiwa rasmi jezi namba 1 tayari kushindania namba na kipa aliyepo klabuni Simon Mignolet.
Kipa huyo Mainz aliweza kukaa Golini na kutofungwa Bao katika Mechi 9 kati ya 34 za Bundesliga akiwa na Mainz akiisaidia klabu hiyo kumaliza katika Nafasi ya 6 katika Msimamo wa Ligi hiyo kuu ya Germany Bundesliga ulioisha hivi karibuni.

No comments