LEO KATIKA HISTORIA : SIMBA YAMPOTEZA PATRICK MAFISANGO MWAKA 2012

Leo katika historia tunakumbuka matukio kadhaa ya soka lakini tukio ambalo litakumbukwa zaidi na mashabiki wa Wekundu wa msimbazi Simba ni kifo cha Nyota wao kiungo raia wa Rwanda Patrick Mutesa Mafisango ambaye alifariki tarehe kama ya leo yani tarehe 17 Mwezi Mei mwaka 2012.


Huyu ndiye Patrick Mafisango 
Mafisango aliyekua akicheza kama kiungo katika timu yake ya Simba na timu ya taifa ya Rwanda  (Amavubi) alikutwa na umauti akiwa na umri wa miaka 32 Chanzo cha kifo chake ni ajali ya gari.
Mafisango alipata ajali hiyo akitokea kwenye Ukumbi wa Starehe wa Club Maisha uliyopo Masaki jijini Dar es salaam na kupata ajali maeneo ya Keko jirani na Chuo cha VETA jijini Dar es Salaam.
Hii ndiyo gari aliyekua akiendesha 
Mafisango alifariki, baada ya gari alilokuwa anaendesha kuacha njia na kugonga mti ulio pembezoni mwa barabara ya Chang’ombe majira ya saa kumi kasorobo alfajiri na kufariki papo hapo.

Ndani ya gari kulikuwa na abiria wengine wanne, lakini aliyekutwa na mauti baada ya ajali hiyo ni Mafisango pekee na Mazishi yake yalifanyika Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako ndiyo alikozaliwa mchezaji huyo.

Mafisango atakumbukwa kwa kuwa kati ya wachezaji walioifunga Yanga bao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu msimu wa 2011/2012.



MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI
AMINA

No comments

Powered by Blogger.