MAN UNITED NA NDOTO YA KUSHINDA 19-0 DHIDI YA BOURNEMOUTH LEO.

Mechi ya kiporo ya ligi kuu nchini England msimu huu ambayo ni ya mwisho msimu huu baada ya kuahirishwa juzi kutokana na sababu za kiusalama baina ya wenyeji Manchester United na AFC Bournemouth.


Ndoto pekee waliyonayo mashabiki wa Man United leo pamoja na benchi zima la ufundi ni kuiona timu yao ikishinda bao 19-0 ili iweze kucheza michuano ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya

Tayari timu nne za juu zimeshajulikana ambazo ni Mabingwa Leicester City,Arsenal, Tottenham Hotspurs na Manchester City huku Manchester United ikishika nafasi ya 5 na njia pekee ya kuifikia nafasi ya nne ni kwa kushinda bao hizo 19-0 ili kuipita Manchester City ambayo ina hazina kubwa ya magoli ya kufunga.

Wapenda Soka wengi wa nasubiri kuona miujiza ikijitokeza hii leo katika kikosi cha kocha Luis Van Gaal katika mechi inayotarajiwa kuanza saa 4 kamili usiku.

No comments

Powered by Blogger.