JOEY BARTON AIREJESHA BURNLEY LIGI KUU ENGLAND
Kiungo wa kimataifa wa zamani wa England na klabu ya Burnley ambaye hufahamika kutokana na fujo zake awapo uwanjani Joey Barton hatimaye amerejea katika ligi kuu ya England kwa msimu ujao akiwa na klabu yake hiyo mpya ya Burnley ambayo jana ili kata tiketi na kuwa timu ya kwanza kupanda ligi kuu.
Burnley imepata nafasi hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya QPR katika dimba la Turf Moor goli pekee La Sam Vokes Dakika ya 61 ya mchezo.
Barton alitemwa na QPR wakati msimu unaanza na akajiunga na Burnley wakati huo hakuna aliyetegemea kama atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaopanda Daraja lakini jana ilidhihirika baada ya matokeo hayo.
Ikiwa imebaki Mechi 1 kwa kila Timu, Burnley wapo kileleni wakiwa na Pointi 90 wakifuatiwa na Middlesbrough na Brighton zenye Pointi 88 kila moja na Timu hizo haziwezi kuipita Burnley kwa vile zitapambana zenyewe katika Mechi ya mwisho.
Timu 2 za kileleni za Championship hupanda Daraja moja kwa moja na Timu ya 3 hupatikana kwa Mechi maalum za mchujo zinazohusisha Timu zitakazomaliza Nafasi za 3 hadi ya 6.

No comments