YANGA KANYAGA TWENDE HAKUNA WA KUWAZUIA. STAND YAKAA 3-1
Mbio za ubingwa kwa vinara wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga zimeendelea kunogeshwa baada ya leo kuibuka na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Chama la Wana Stand United.
Pambano hilo lililopigwa katika dimba la Kambarage mjini Shinyanga lilionyesha njia thabiti ya mabingwa hao watetezi kuweza kuutetea ubingwa wao
Dakika ya 3 tu ya mchezo tayari Yanga walishapata bao la uongozi asante kwa shuti la mbali la mshambuliaji Donald Ngoma ambaye aliongeza bao la pili kabla ya mapumziko kufuatia juhudi zake binafsi zilizopelekea kupatikana kwa bao hilo.
Mpaka mapumziko magoli hayo mawili tayari yalishaihakikishia Yanga kuibuka na ushindi katika mechi hiyo lakini Amiss Tambwe aliongeza bao la 3 kwa Yanga kabla ya Elias Maguli hajaipatia Stand United bao la kufutia machozi kwa njia ya penati.
Kwa matokeo hayo sasa Yanga wanaendelea kuongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 68 katika msimamo wa ligi hiyo wakati Stand United wanabaki na pointi zao 31 katika nafasi ya 7.

No comments