EPL MECHI ZA MWISHO : ARSENAL YAPANDA NAFASI YA PILI,SPURS YAPIGWA 5 MAN CITY YATINGA MABINGWA ULAYA

Mechi za mwisho za ligi kuu nchini England zilipigwa jana kwa timu zote kucheza isipokua mechi moja tu kati ya Manchester United na AFC Bournemouth ambayo iliahirishwa kutokana na tishio la Bomu uwanjani.


Arsenal iliikandamiza Aston Villa bao 4-0 katika pambano lililopigwa katika dimba la Emirates ikiwa ni mechi ya kumuaga Thomas Rosisky  baada ya kudumu na washika bunduki hao wa London kwa miaka 10 na kupanda mpaka nafasi ya pili.

Manchester City wao wakiwa ugenini walitoka Sare ya bao 1-1 na Wenyeji Swansea City Sare ambayo inawafanya kutinga katika ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao kwakua wapinzani wao Manchester United ambao jana hawakucheza wanatakiwa kushinda si chini ya bao 19-0.

Mabingwa wapya Leicester City wao walitoka suluhu na Chelsea katika mchezo uliopigwa katika dimba la Stamford Bridge  jijini London.

Tottenham Hotspurs ambao walikua katika mbio za kusaka ubingwa msimu huu wamejikuta wanaambulia nafasi ya tatu baada ya kulambishwa bao 5-1 na timu iliyoshuka Daraja.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA JANA EPL

  • Arsenal 4-0 Aston Villa 
  • Chelsea 1-1 Leicester City 
  • Swansea 1-1 Man City 
  • West Brom 1-1 Liverpool 
  • Newcastle United 5-1 Tottenham Hotspurs 
  • Everton 3-0 Norwich City 
  • Southampton 4-1 Crystal Palace 
  • Stoke City 2-1 West Ham 
  • Sunderland 2-2 Watford 

No comments

Powered by Blogger.