BANDA AIBEBA SIMBA DHIDI YA MTIBWA, AZAM YAIZAMISHA AFRICAN SPORTS

Baada ya matokeo mabaya kwa Wekundu wa Msimbazi Simba katika mechi zao 5 zilizopita hatimaye jana Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa sugar.


Shujaa wa pambano hilo ni kiungo aliyekua na mgogoro na kocha wa klabu hiyo Abdi Banda akifunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi ya beki wa kushoto wa Simba Mohamed Hussein Tshabalala

Pambano lingine katika ligi hiyo jana wenyeji African Sports walilambishwa bao 2-1 na wana lamba lamba Azam FC.

Allan Wanga na Erasto Nyoni wakiwa ndiyo wafungaji wa mabao hayo ya Azam FC kipigo ambacho kinaifanya African Sports kusubiri kudra za Mwenyezi Mungu kuendelea kucheza ligi kuu msimu ujao.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA JANA VPL


No comments

Powered by Blogger.