BAYERN MUNICH YAMNASA KIUNGO ALIYEKUWA KATIKA RADA ZA MAN UNITED
Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich leo wamekamilisha usajili wa kiungo wa Benfica Renato Sanchez na Mlinzi wa Borussia Dortmund Matts Hummels.
Hili ni Pigo kwa Manchester United ambao wamekuwa wakihusishwa kwa kiwango kikubwa kumwania Nyota huyo raia wa Ureno.
Habari kutoka Ujerumani zinasema staa huyo mwenye umri wa miaka 18 amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuichezea miamba hiyo ya Bundesliga na atakua chini ya kocha Carlo Ancelotti ambaye atachukua nafasi ya Pep Guardiola anayetimkia Man City.
Sanches amejiunga na Bayern Munich kwa ada ya awali ya €35m ambayo itapanda na kufikia £63m.
Bayern pia wamemtangaza Matts Hummels kama mchezaji wao baada ya kumsajili toka Borussia Dortmund kwa mkataba wa miaka mitano pia.

No comments