HAWABEBEKI : MAN UNITED YADUNDWA NA WEST HAM NA KUPOTEZA MATUMAINI YA TOP 4

Ni kama hawabebeki ndivyo unavyoweza kusema kwa kikosi cha Luis Van Gaal kwani kazi pekee waliyokua nayo ilikua ni kushinda mechi dhidi ya West Ham kisha kushinda Mechi ya mwisho dhidi ya Bournemouth ili kutinga katika Top 4.

Hali imekua tofauti baada ya West Ham kuifunga ManchesterUnited bao 3-2 na kupoteza kabisa matumaini ya kuwa miongoni mwa timu zitakazomaliza katika nafasi nne za juu.

Diafra Sakho alitangulia kufunga bao la kwanza kwa West Ham goli ambalo lilidumu mpaka mapumziko. 

Na kipindi cha pili ndicho kiliwaacha mashabiki wa Man United midomo wazi kwani kilichanganyika na kicheko na kununua Antony Martial akifunga bao la kusawazisha kisha kuongeza la pili lakini Antonio na Winston Reid waliharibu kila aina ya furaha kwa Mashabiki wa Manchester United baada ya kufunga bao mbili zilizoipa ushindi West Ham.

Kwa matokeo hayo sasa Manchester United wanaendelea kukamata nafasi ya 5 wakiwa na pointi 63 wakati West Ham wanakamata nafasi ya 6 na pointi 62.

Njia pekee kwa United kuingia top 4 ni kuombea Man City ifungwe ugenini dhidi ya Swansea kisha Yenyewe ishinde dhidi ya Bournemouth nyumbani ili kushika nafasi ya Top 4.

No comments

Powered by Blogger.