MARTIAL AFUNGA BAO LA KIHISTORIA WAKATI DIMBA LA OLD TRAFFORD LIKIMTUNUKU SIR BOBBY CHALTON

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea Manchester United Antony Martial leo ameingia katika kumbukumbu muhimu kwa klabu hiyo baada ya kufunga bao pekee katika mchezo wa ligi kuu nchini England dhidi ya
Everton katika dimba la Old Trafford





Manchester United iliibuka na ushindi wa bao hilo 1  katika mechi ambayo legendari wa klabu hiyo Sir Bobby Chalton alitunukiwa heshima ya pekee akiungana na Sir Alex Ferguson kuandikwa katika majukwaa ya klabu hiyo na kupewa jukwaa la kusini lililoandikwa JUKWAA LA SIR BOBBY CHALTON (SIR BOBBY CHALTON STAND)

Martial alifunga bao hilo pekee na kumfanya kutinga katika kumbukumbu ya kuwa mchezaji wa Man United aliyefunga bao la 1000 katika ligi kuu ya England katika dimba la Old Trafford tangu msimu mpya wa ligi ulipoanzishwa mwakati 1992.

Tumekuwekea hapa picha za matukio ya mchezo huo

Sir Bobby Chalton na Mkewe kabla ya mchezo huo 


Jukwaa la Bobby 


Wayne Rooney akiwa jukwaani 

Roberto Martinez kocha wa Everton 

Rashford akiwatoka Jagielka na Banes 


Lingard akimzuia Rose Barkley


Martial akimtoka Stones


De Gea kazini


Wachezaji wa United wakishangilia


No comments

Powered by Blogger.