YANGA YAIKANDAMIZA KAGERA WAKATI AZAM WAKILAZIMISHWA SARE NA TOTO
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania bara Yanimeishushia kipigo cha bao 3-1 Kagera Sugar kutoka Mkoani Kagera.
Pambano hilo la Ligi kuu nchini Tanzania lilipigwa katika dimba La Taifa Jijini Dar es Saalm likishuhudia Kagera Sugar ambao wanapigania kubaki katika ligi kuu wakipata bao la mapema kupitia kwa Mubarak Yusuph.
Donald Ngoma aliisawazishia Yanga kabla ya Amiss Tambwe hajaongeza bao la pili na Haji Mwinyi akafunga bao la Tatu na kuihakikishia Yanga pointi tatu muhimu leo.
Jijini Mwanza wenyeji Toto African ya Mwanza waliisimamisha Azam FC iliyosafiri kusaka pointi 3 kwa kwenda Sare ya bao 1-1 katika mchezo uliopigwa katika dimba la CCM KIRUMBA ambalo lilijaa Maji kutokana na mvua iliyonyesha na kusababisha ladha ya mchezo huo kupotea
Azam FC walitangulia kupata bao kupitia kwa nahodha John Bocco kabla ya Toto Africans kusawazisha kwa bao lililofungwa na Wazir Junior.
Matokeo mengine jana Stand waliisambaratisha Mgambo JKT kwa kuilaza bao 2-0 wakati Ndanda FC wakiwa nyumbani walitoka Sare ya bila kufungana na Prisons ya Mbeya.
JKT Ruvu wakiwakaribisha African Sports waliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Kwa matokeo hayo bado Simba wanaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 57 wakifatiwa na Yanga wenye pointi 53 huku Azam wakikamata nafasi ya 3 na pointi zao 51.
Coastal Union wanashika mkia wakiwa na pointi 19 wakifatiwa na ndugu zao African Sports wenye pointi 20.

No comments