SIMBA YARUDI KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA
Wekundu wa msimbazi Simba wamerudi kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuikandamiza Mbeya City bao 2-0.
Kazi kubwa iliyofanywa na Ibrahim Ajib ilizaa magoli yote mawili yakipatikana dakika za mwishoni za kipindi hicho baada ya kuwalamba chenga mabeki wa Mbeya City kisha Danny Lyanga akifunga bao la kwanza na bao la pili Ajib akifanya vile vile kama alivyofanya na safari hii beki wa Mbeya City akajifunga wakati akitaka kuokoa.
Kwa matokeo hayo Simba sasa wanarudi juu katika msimamo wa ligi hiyo wakifikisha pointi 48 pointi moja mbele ya Azam FC na Yanga SC wenye pointi 47 japokua Simba ina mchezo mmoja mbele yao.

No comments