VINARA LEICESTER CITY WAZIDI KUKIMBIZA ENGLAND,ARSENAL,SPURS NA CHELSEA ZAAMBULIA SARE.

Hatua ya 29 ya ligi kuu nchini England ilianza jana kwa mechi 8 kupigwa katika viwanja tofauti nchini humo.



Vinara wa ligi hiyo klabu ya Leicester city wakiwa ugenini katika mechi ya mwisho hiyo jana wakiifunga Watford kwa bao 1-0 katika pambano ambalo kiungo kisiki wa timu hiyo N'golo Kante alirejea Uwanjani baada ya kukosa mechi iliyopita.
Bao pekee La Leicester City likifungwa na winga wa kimataifa wa Algeria Ryad Mahrez.

Katika mechi ya mapema hiyo jana Tottenham Hotspurs wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani White Hart Lane walilazimishwa Sare ya bao 2-2 na Arsenal. Arsenal walitangulia kupata bao lililofungwa na Aaron Ramsey kabla ya Toby Andelweid hajaisawazishia Spurs na Harry Kane akaongeza bao la pili kabla ya Alexis Sanchez hajaisawazishia Arsenal na kufanya mchezo huo kumalizika kwa Sare hiyo.

Katika mchezo mwingine hiyo jana Chelsea walishikwa shati na Stoke na kalazimishwa Sare ya bao 1-1 Chelsea walitangulia kufunga kupitia kwa beki wake Traore kabla ya Diouf hajaisawazishia Stoke City  katika mchezo uliopigwa katika dimba La Stamford Bridge.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA JANA EPL


  • Tottenham 2-2 Arsenal 
  • Chelsea 1-0 Stoke City 
  • Everton 2-3 West Ham 
  • Man City 4-0 Aston Villa 
  • Newcastle 1-3 Bournemouth 
  • Swansea 1-0 Norwich 
  • Southampton 1-1 Sunderland 
  • Watford 0-1 Leicester 

No comments

Powered by Blogger.