LICHA YA KUTOKA SARE TAIFA YANGA YAITUPA NJE APR YA RWANDA

Mabingwa wa Tanzania bara Yanga SC wametinga hatua ya pili ya michuano ya klabu bingwa Africa baada ya kutoka Sare ya bao 1-1 na mabingwa wa Rwanda klabu ya APR.



Katika mchezo huo wa marudiano wa hatua ya kwanza uliopigwa katika dimba la Taifa Jijini Dar es salaam Yanga ilikua ikihitaji Sare tu ili kuvuka baada ya kushinda katika mechi ya awali kule Kigali kwa bao 2-1 hivyo kuvuka kwa ushindi wa Jumla wa bao 3-2.

APR walitangulia kupata bao la mapema kupitia kwa Fiston Nkinzingabo akimalizia pasi ya Jean Claude Iranzi lakini Yanga walicharuka na kusawazisha bao hilo likifungwa na Donald Ngoma ambaye ni Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe.

Kwa matokeo hayo sasa Yanga wanakutana na Mshindi kati ya Recreativo de Libolo ya Angola na Al Ahly ya Misri.

No comments

Powered by Blogger.