SIMBA HAIZUILIKI LIGI KUU YAZIDI KUTEMBEZA VICHAPO, KIIZA HATARI TUPU.
Wekundu wa Msimbazi Simba ambao ni vinara wa ligi kuu Tanzania bara wameendeleza vipigo kwa kila timu wanayokutana nayo na hii leo wakishusha kichapo kwa Coastal Union ya Tanga.
Simba imeibuka na ushindi wa bao 2-0 katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga.
Hamis Kiiza ambaye ni Kinara katika kupachika mabao alifunga bao lake la 19 msimu huu kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi ya Nimuboma likiwa ni bao la pili kwa Simba katika mchezo wa leo likitanguliwa na lile la kwanza lililofungwa na Mshambuliaji wa zamani wa Coastal Union Anayeichezea Simba hivi sasa Danny Lyanga akiunganisha mpira wa krosi ya Mohamed Hussein Tshabalala.
Kwa matokeo hayo Simba wanafikisha Pointi 57 katika nafasi ya kwanza zikiwa ni pointi 7 zaidi ya Azam na Yanga wenye pointi 50 huku Simba ikiwazidi michezo mitatu.
![]() |
Danny Lyanga akishangilia bao alilofunga |

No comments