LEICESTER CITY YAZIDI KUKUSANYA POINTI KILELENI,ARSENAL YAMALIZIA HASIRA KWA EVERTON.

Vinara wa ligi kuu nchini England Leicester City imeendelea kujikusanyia pointi katika mfululizo wa mechi za ligi kuu nchini England baada ya kuchapwa Crystal Palace kwao.



LEICESTER CITY  ambayo matokeo yake msimu huu hayakutegemewa na wengi imekomaa na kuzoa pointi zote tatu ugenini kwa kuifunga Crystal Palace bao  1-0 goli pekee katika mchezo huo likifungwa na winga wa kimataifa wa Algeria Ryad Mahrez akitumia vyema pasi ya Jermie Vardy.

Ushindi wa Leicester City leo umezidi kutoa mwangaza kwa klabu hiyo kuweza kunyakua taji lake la kwanza katika ligi kuu ya England ikifikisha sasa pointi 63 katika nafasi ya kwanza.

Katika mechi nyingine leo Watford wakiwa nyumbani walifungwa bao 2-1 na Stoke City na West Bromwich Albion wakakubali kichapo cha bao 1-0



No comments

Powered by Blogger.