KIPRE TCHETCHE APIGA HAT-TRICK AZAM IKISONGA MBELE KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Wawakilishi wa Tanzania bara katika michuano ya kombe la shirikisho barani Africa Azam FC imeibuka na ushindi wa bao 4-3 nyumbani dhidi ya Bidvest ya Afrika Kusini.





Mchezo huo wa raundi ya kwanza uliopigwa katika dimba la Azam Complex Mbagala jijini Dar es salaam ulikua ni wa marudiano baina ya timu hizo baada ya mechi ya awali kule Afrika Kusini kushuhudia Azam ikiibugiza Bidvest bao 3-0.

Shujaa wa mchezo wa leo alikua Mshambuliaji wa Ivory Coast anayekipiga Azam FC Kipre Herman Tchetche aliyefunga mabao matatu peke yake huku Nahodha John Bocco akifunga pia bao moja.

Kwa matokeo hayo Azam fc wamevuka hatua hii ya kwanza ya michuano hiyo ambayo ni ya pili kwa ukubwa Afrika katika ngazi ya klabu na sasa wanakutana na Esperance ya Tunisia katika hatua inayofata  mechi ya kwanza ikipigwa Dar es salaam wiki mbili zijazo.

1 comment:

Powered by Blogger.