TIMU ZA MADRID ZAISAFISHIA BARCELONA NJIA YA UBINGWA LA LIGA.
Sare walizopata Real Madrid na Atletico Madrid jana huenda zikawa njia nzuri zaidi ya Barcelona kutetea ubingwa wao wa ligi kuu nchini Spain La Liga.
Ikicheza ugenini Real Madrid ilishindwa kupata pointi 3 dhidi ya Malaga huku Cristiano Ronaldo licha ya kufunga bao pekee lakini akishindwa kufunga penati ambayo Real Madrid waliipata.
Atletico Madrid wakiwa nyumbani walitoka sare tasa ya bila kufungana na Villareal katika dimba la Calderon na kuzidi kujiweka pabaya katika kuwania ubingwa wa La Liga kwani sasa Barcelona ambao waliifunga Las Palmas Jumamosi bao 2-1 na kuendelea kushika uongozi wa ligi hiyo wakiwa na pointi 63 wakati Atletico Madrid wanashika nafasi ya pili na pointi 55 na Real Madrid nafasi ya tatu wakiwa na pointi 54.

No comments