MAN UNITED YAZINDUKIA KOMBE LA FA YASHINDA 3 UGENINI

Mechi za Hatua ya Tano ya michuano ya kombe la Chama cha soka nchini England maarufu kama kombe la FA zimekamilika usiku huu kwa Manchester United kuifunga Shrewsbury bao 3-0



United ambayo ilipoteza mchezo uliopita wa michuano ya kombe la Europa kwa kuchapwa  na Midtjylland ya Denmark bao 2-1 ilionyesha uhai katika mechi hii na kufanikiwa kupata mabao mawili mpaka half time.

Chris Smalling na Juan Mata wakitangulia kuifungia United kipindi hicho cha kwanza kabla Jesse Lingard hajafunga bao la tatu na kutupwa kabisa nje timu hiyO ya Shrewsbury

Kwa matokeo hayo Man United itacheza na West Ham katika mechi ya hatua ya robo fainali.

No comments

Powered by Blogger.