CHELSEA KUWAVAA EVERTON, MAN UNITED IKIVUKA LEO KUKUTANA NA WEST HAM

Ratiba ya Mechi za hatua ya robo fainali ya kombe la Chama cha soka nchini England Maarufu kama kombe la FA zimepangwa jana usiku baada ya mechi ya Chelsea na Manchester City na kushuhudia Chelsea wakiibugiza Man City bao 5-1.



Ratiba inaonyesha Chelsea watasafiri kuwakabili Everton katika uwanja wa Goodson Park timu ambayo imetinga hatua hii baada ya kuwalaza Bournemouth bao 2-0 magoli ya Romelu Lukaku na Rose Barkley.

Manchester United ambayo inacheza usiku wa leo na timu ya Shrewsbury  kama itaputa hatua hii itacheza na West Ham ambao jana waliwabugiza Blackburn Rovers bao 5-1 katika mechi ya raundi ya 5.

Mabingwa watetezi Arsenal ambao watatakiwa kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Hull City baada ya kutoka sare ya bila kufungana kama watavuka hatua ya Tano watakutana na Watford
Ambao wamevuka baada ya kuwaondosha Leeds United kwa bao 1-0.

Reading ambao waliwaondosha West Bromwich Albion kwa kuwalamba bao 3-1 watacheza na Crystal Palace ambao jana waliwatupa nje Tottenham Hottspurs.

Mechi za hatua ya Robo fainali zitachezwa wikiend ya tarehe 11-14 mwezi March 2016.

No comments

Powered by Blogger.