SIMBA YAMALIZIA HASIRA ZAKE KWA SINGIDA UNITED,YAIPA MKONO


Wekundu wa Msimbazi SIMBA leo wamepoza machungu ya kufungwa na Yanga baada ya kuifumua Singida United "mkono" yani bao 5-1.




Mchezo huo wa kombe La Shirikisho nchini ulipigwa katika dimba La Taifa Jijini Dar ikiwa ni tiketi ya kutinga hatua ya Robo fainali ya michuano hiyo ambayo bingwa wake ataiwakilisha nchi katika kombe La Shirikisho barani Africa.

Magoli ya simba leo yalifungwa na Hamis Kiiza aliyefunga mabao mawili huku Awadh Juma naye akifunga mawili na Danny Lyanga naye akifunga bao moja wakati lile La Singida United likiwekwa kimiani na Paul Malamla.

Katika mechi nyingine leo Geita Gold waliitandika Toto African ya Mwanza bao 1-0 goli pekee likifungwa na Chibuga Chibuga aliyeunganisha pasi ya Juma Nade.

Kwa matokeo hayo ya leo SIMBA na Geita wanaungana na timu za Yanga,Ndanda FC,Coastal Union na Mwadui ambao tayari wameshafuzu.

No comments

Powered by Blogger.