SIMBA YAENDELEZA DOZI TAIFA,SAFARI HII YAIPIGA MGAMBO "MKONO"

Dozi zimeendelea kutolewa  na Simba Sc katika mashindano mbalimbali ikiwa na kocha wake mpya Jackson Mayanja baada ya jioni hii kuifumua  Mgambo JKT bao 5-1


Simba ambayo haijawahi kufungwa mchezo wowote chini ya kocha Mayanja imeonekana kuzidi Kuimarika baada ya kutoa kichapo hicho kwa Mgambo katika mfululizo wa mechi za ligi kuu Tanzania bara

Pambano hilo lililopigwa  katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam na kuvuta  hisia za mashabiki wengi ilishuhudia Hamis Kiiza akifunga bao la mapema kabisa baada ya kutumia udhaifu  wa mabeki wa Mgambo na kufunga kabla ya Mwinyi Kazimoto na Ibrahim Ajib hawajafunga  na mchezo huo kwenda mapumziko matokeo yakiwapa ushindi  Simba wa bao 3-0.

Kipindi cha pili Simba walikianza taratibu  huku wakimtumia sana Mkude na Majabvi kutibua mipango ya Mgambo na kufanikiwa kupata mabao mawili zaidi moja likifungwa na Danny Lyanga na Hamis Kiiza huku Mgambo nao walijitutumua na kufunga bao pekee kupitia kwa Fulyzulu  Maganga

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 39 sawa na Azam fC lakini Azam wao wana faida ya mechi mbili mkononi  baada ya mechi zao kusogezwa  mbele huku Yanga ambao wamelazimishwa sare na Prisons http://wapendasoka.blogspot.com/2016/02/penati-yaiokoa-yanga-isipate-kipigo.html ikiongoza ligi ikiwa na pointi 40

No comments

Powered by Blogger.