RONALDO APIGA HAT-TRICK REAL MADRID IKISHINDA BAO 6-0

Mechi ya  ligi kuu nchini Spain baina ya Real na Espanyol imemalizika  kwa Real Madrid  kuibuka na ushindi mnono wa bao 6-0




Cristiano Ronaldo alifunga mabao matatu yani hat-trick katika mchezo huo huku magoli ya Karim Benzema,James Rodriguez na goli la kujifunga  la mlinzi wa Espanyol Oscar Duarte yakikamilisha ushindi huo mnono kwa Real Madrid wanaonolewa  na Zinedine Zidane.

Tangu Zinedine aanze kuifundisha  Real Madrid timu hiyo haijafungwa  na kwa matokeo hayo Real Madrid inaendelea kushika nafasi ya 3 ikiwa na pointi zake 47 pointi moja nyuma ya Atletico Madrid wanaokamata nafasi ya pili.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA JUMAPILI

  • Real Madrid 6-0  Espanyol 
  • Sevilla 3-1 Levante 
  • Valencia 0-1 Sporting Gijon 
  • Las Palmas 2-1 Celta Vigo

No comments

Powered by Blogger.