CHELSEA YAIBAMIZA MK DONS MKONO, EVERTON NAO WAMO

Chelsea imetinga hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la chama cha soka nchini England FA baada ya kuibamiza  MK  Dons bao 5-1.




Mchezo huo wa Raundi  ya nne ya michuano hiyo ilishuhudia  Chelsea wakipata mabao yao kupitia kwa Oscar aliyefunga bao 3 peke yake huku Eden Hazard  akifunga bao pia kwa Chelsea na lingine moja  likifungwa na Bertrand Traore

Katika mchezo wa awali Everton ikiwa nyumbani  Goodson Park ikiibuka na ushindi wa bao 3-0 ikiifunga  Carlisle United

Aruna Kone,Aaron Lenon  na Rose Barkley wote walifunga bao moja moja na kuifanya Everton kati ya timu 16 zitakazopambana  hatua inayofata.

No comments

Powered by Blogger.