YANGA YAFUNGULIA VIPIGO TANGA, YALAMBISHWA 2 NA COASTAL UNION
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga leo wameambulia kichapo cha bao 2-0 toka kwa Wagosi wa Ndimba Coastal Union ya Tanga katika dimba la Mkwakwani.
Yanga ambao wanaongoza ligi kuu licha ya kufungwa walijikuta wakipoteana kabisa na kukubali kichapo hicho magoli ya Coastal Union yakifungwa na Miraji Adam na Juma Mahadhi.
Hii ni mechi ya kwanza kwa Yanga kufungwa msimu huu na pengine inaweza ikawa imefungulia vipigo kama haitajirekebisha katika mechi inayofata.
MATOKEO YA MECHI ZA LEO VPL
Simba SC 4-0 African Sports
Coastal Union 2-0 Yanga SC
JKT Ruvu 0-0 Maji maji
Mwadui 1-0 Toto Africans
No comments