WALICHOFANYIWA AFRICAN SPORTS NA SIMBA TAIFA HAWATAKAA WASAHAU

African Sports ya Tanga  kwa mara ya kwanza  Ikicheza  katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam  tangu kuanzishwa  kwake ilijikuta ikipigwa bao 4-0.




Simba SC  ambayo  inaendeleza Wimbi  lake la ushindi  chini ya kocha Jackson Mayanja Ikicheza mechi ya tatu katika ligi na kupata ushindi huo mnono.

Hamis Kiiza alifunga mabao mawili, Hassan Kessy  na Haji  Ugando  waliifunga Simba bao moja moja na kufanya  mchezo huo  kumalizika kwa ushindi wa bao 4-0  ambao Simba walipata.

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha  pointi 36 katika nafasi ya tatu  pointi 3 nyuma ya Yanga na Azam zinazoongoza  ligi hiyo.

Hii ni mechi ya nne kwa kocha mpya wa Simba Jackson Mayanja  katika mashindano yote kwanza aliamua na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa, Akawafunga  Jkt Ruvu  bao 2-0 Kisha Akawafunga Burkina Faso  bao 3-0 katika kombe la Shirikisho na leo kushinda bao 4-0 dhidi ya African Sports.
Amefunga magoli 10 na hajafungwa goli lolote.

No comments

Powered by Blogger.