YANGA YAFANYA ILICHOKIFANYA SIMBA JANA, YAIPIGA 3 RANGERS

Mabingwa wa Tanzania bara Yanga wameanza vizuri kampeni yao ya kuwania ubingwa wa kombe la Shirikisho nchini Tanzania kwa kuibuka na ushindi mnono dhidi ya Friends Rangers.


Yanga imeibuka na ushindi wa bao 3-0 ushindi sawa na ule walioupata Simba jana huko Morogoro dhidi ya Burkina Faso ya Morogoro.

Simon Msuva aliongoza mashambulizi leo dhidi ya timu hiyo ya daraja la kwanza kwa kufunga Mabao mawili huku Mshambuliaji Mateo Anthony akifunga bao moja.

Mechi hiyo ni ya Raundi ya 3 na kuifanya Yanga kuvuka kuingia hatua ya nne ambayo itashirikisha timu 16 bora. Bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

No comments

Powered by Blogger.