USAJILI BORA WA MSIMU KATIKA LIGI KUU YA ENGLAND

Tumekuandalia listi ya wachezaji waliosajiliwa na kufanya vizuri katika ligi kuu nchini England mpaka sasa wakati ligi hiyo ikiwa katika hatua ya lala salama


1. Georginio Wijnaldum
Kiungo mshambuliaji wa Newcastle United aliyesajiliwa kutoka PSV ya Uholanzi akicheza kama kiungo katika klabu ya Newcastle United ameshafunga magoli 9 na kusaidia mengine 3. Wijnaldum amkeuwa ni chachu ya Newcastle kufanya vizuri katika msimu huu.





2. Petr Cech
Akiwa ndiyo kipa rekodi nzuri ya nyavu zake kutotikiswa msimu huu. amechezwa mechi 10 bila nyavu zake kutikiswa na kuwa mchezaji bora wa mechi katika mechi 3 kwa msimu huu.



3. Andrew Ayew
Ameisaidia Swansea kupata points  muhimu sana msimu huu, zikiwapo kati ya Chelsea, United na Tottenham. Na pia ana magoli 8 na kusaidia mengine 3.









4. Kevin De Bruyne
Chelsea walimuuza kwa £18m lakini miezi 19 baadae kiwango chake pale Bundes Liga kimepandisha thamani yake mpaka £54.5m na kuweka rekodi. Amefunga magoli 12 katika mashindano yote  na kusaidia mengine 9, amechukua tuzo 2 za mcezaji bora wa mechi. Na tukumbuke ana miaka 24 tu.


5. Raheem Sterling
Alifunga hat-trick dhidi ya Bournemouth, jumla kafunga magoli 9 katika mashindano yote na kusaidia mengine 3. Pia amechukua tuzo 3 za mchezaji bora wa mwezi.





6.Toby Alderweireld
Mpaka sasa Spurs wana beki imara zaidi pale katika ligi kuu uingereza, wakiwa wameruhusu magoli 19 tu. Moja ya uimara wa beki hii ni sababu ya uwepo na Toby. Pia amefunga magoli 2 na kuassist mara 3.



7. Anthony Martial
Ndiyo usajili ghali zaidi kwa majira ya joto, alinunuliwa toka Monaco kwa gharama ya £57.6m na makali yake yalianza kuonekana haraka katika mechi yake ya kwanza dhidi ya mahasimu wakubwa wa United, Liverpool. Katika mashindano yote amefunga magoli 8 na kusaidia mengine 4.



8. Christian Benteke.
Klop bado hajamuamini sana Huyu Mbelgiji, lakini ameshafunga mara 7 na kuassist mara 5 katika mashindano yote pia amechukua tuzo 3 za mchezaji bora wa mechi.




9. Dimitri Payet.
Kwangu ni moja ya kipaji bora kabisa kuja EPL. Westham walilitoa £10m kumtoa Marseille,
Amekuwa ni nguzo kwa Westham hasa katika nafasi ya kiungo . Mpaka sasa amefunga mara 6 na kuassist mara 4.





10. Glen Johnson
Alishindwa kung'ara pale Liverpool msimu ulopita, akaenda bure pale Stoke city. Uhamisho wake umelipa, ameisaidia Stoke hasa kipa wao kua na Cleansheet 9, rekodi safi nyuma ya zile 10 za Cech. Lakini pia amesaidia magoli 3.




Ni hayo tu kwa leo.

Imeandaliwa na
~ Dennis Kayoka kutoka Wapenda Soka Tanzania

■ SOKA LETU | JAMII YETU ■

No comments

Powered by Blogger.