SAMATTA ATAMBULISHWA RASMI GENK A PESA JEZI NAMBA 77

Klabu ya Krc Genk ya Ubelgiji Imemsajili rasmi Mshambuliaji na kapteni wa team ya taifa ya Tanzania  aliyekua anaichezea klabu ya Tp mazembe ya Congo Mbwana  Ally  Samatta katika Dirisha dogo la usajiri wa Januari


Mbwana Ally Sammatta mwenye umri wa miaka 24 amejiunga rasmi na klabu hiyo Inayoshiriki ligi kuu ya Ubelgiji  akitokea Tp Mazembe ambako mkataba wake ulikua umebaki miezi sita na amesaini mkataba wa miaka minne kuitumikia klabu hiyo iliyotoa nyota kadhaa barani Ulaya.

Genk inashika  nafasi ya 6 katika  msimamo  wa ligi ya Ubelgiji ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza mechi 23. Timu inaongozwa ni AA Gent yenye pointi 49 ikifatiwa na Club Brugge  yenye pointi 46

Samatta alipoulizwa  kwanini kachagua  namba 77 alisema hataki  kushindania  namba 7 ambayo walimpa  avae kwani duniani kote namba 7 inagombaniwa

No comments

Powered by Blogger.