SUAREZ APIGA HAT-TRICK BARCELONA IKIMPONGEZA MESSI KWA BAO 6-0.


Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez jana usiku alipiga bao tatu katika ushindi wa bao 6-0 walioupata Barcelona dhidi ya Athletic Bilbao.




Pambano hilo la ligi kuu ya Spain lilikua mahususi kumpongeza Messia kwa kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia kwa mara ya Tano katika historia ambapo alipata fursa ya kuwaonyesha mashabiki katika dimba la Nou Camp tuzo hiyo kabla ya mechi.

Katika mechi hiyo Athletic Bilbao walishindwa kabisa kuzuia kasi ya washambuliaji nyota wa Barcelona Messi,Suarez na Neymar na kuruhusu Suarez kufunga mabao matatu na kusaidia kupatikana bao moja,Messi akafunga bao moja kwa njia ya penati huku Neymar akifunga bao moja na kusaidia kupatikana mabao mawili na bao lingine likifungwa na Ivan Rakitic.

Kwa matokeo hayo Barcelona wamebaki katika nafasi ya pili nyuma ya Atletico Madrid.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA JANA LA LIGA

Valencia 2-2 Rayo Vallecano

Real Madrid 5-1 Sporting Gijon

Getafe 3-1 Espanyol

Las Palmas 0-3 Atletico Madrid

Barcelona 6-0 Athetic Bilbao

No comments

Powered by Blogger.