GOLI LA KIIZA LAIBEBA SIMBA TAIFA, YALIPIZA KISASI KWA MTIBWA.

Goli la dakika ya 5 la mshambuliaji Wa Simba Raia wa Uganda Hamis Kiiza limeibeba Simba katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.




Simba ambao walicheza kwa kasi dakika 45 za kipindi cha kwanza tofauti na mechi zao zilizopita waliweza kuwakamata vilivyo Mtibwa hasa eneo la katikati ya uwanja Justice Majabvi na Jonas Mkude wakisaidiwa na Mwinyi Kazimoto wakifanya kazi ya ziada kuwapoteza kabisa Mtibwa ambao katika mechi ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi.

Hamis Kiiza alifunga bao hilo pekee kwa kichwa akiunganisha pasi ya Mohamed Hussein Tshabalala na kumwacha kipa kipa Wa Mtibwa Nduda akiruka bila mafanikio.

Kwa matokeo hayo Simba wamefikisha pointi 30 katika nafasi ya 3 ikiwa ni pointi 3 nyuma ya watani wao Yanga ambao kesho watacheza dhidi ya Ndanda FC


MATOKEO YA MECHI ZA LEO TANZANIA BARA

Simba 1-0 Mtibwa
Mbeya City 1-0 Mwadui FC
Stand United 1-0 Kagera Sugar
Coastal Union 1-1 Maji Maji FC
JKT Ruvu 1-5 Mgambo JKT

No comments

Powered by Blogger.